Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye akitoa shukrani zake za pekee kwa kampuni ya GroovJoint iliyokuja nchini Tanzania kuwekeza upande wa viunganishi vya mabomba ambapo alisema kuwa wameamua kuwapokea kwa mikono miwili kampuni hiyo kwa vile viunganishi vitasaidia wananchi kupata maji safi na salama. Pembeni ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani iliyokuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya viwanda na Wakala wa wauzaji wa Vifaa Vya kuunganishia mabomba yanayotoka nchini Marekani, David Robert Mwamsojo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye akimshukuru Makamu wa Rais wa Kampuni ya GroovJoint ya nchini Marekani, David Newman mara baada ya mkutano na waandishi wa habari kuelezea malengo ya kampuni yao. Pembeni ni Wakala wa wauzaji wa Vifaa Vya kuunganishia mabomba yanayotoka nchini Marekani, David Robert Mwamsojo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...