Wadau wa habari nchini wameomba kupata taarifa iwe ni haki ya kila mtu ambayo inapaswa kulindwa kwa nguvu zote na ni kiashiria kimoja wapo cha serikali yenye uwazi na inayothamini mchango na ushiriki wa wananchi wake katika ujenzi wa taifa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji wa habari yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, wamesema kila mtu ana haki ya kupokea na kutoa taarifa ili mradi tu asiende nje ya swala husika.
Wamesema kuwa, lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya haki ya kila mtu na kupata taarifa muhimu kwa Maisha yao ikiwa ndani ya hifadhi ya Serikali na kwingineko, namna viongozi waliyochaguliwa na wanavyotekeleza majukumu yao.
Katika maadhimisho hayo MISA-TAN walikabidhi tuzo kwa taasisi mbali mbali za umma zinazotoa taarifa kwa uwazi na zile zinazobana taarifa. Kwa mwaka 2017, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeibuka mshindi wa kwanza kwa utoaji na upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma na taasisi iliyokuwa mshindi wa mwisho ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) baada ya kubainika kuwa inabana taarifa. Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Kila Mtanzania Anayo Haki Ya Kupewa Taarifa."
Wageni waalikwa wakisimama kwa kuwakumbuka waandishi waliyopoteza maisha katika maadhimisho ya kwanza Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Taarifa yaliyofanyika leo Dar es Salaam, Tanzania.
Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI), Kajubi Mukajanga akiakitoa utangulizi kuhusu upatikanaji wa taarifa kwa wananchi nchini Tanzania kwenye siku ya maadhimisho ya kimataifa ya upatikanaji wa taarifa leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali wachangia mada kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upatikanaji wa habari.
KWA PICHA ZAIDI BODYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BODYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...