Na Fatma Salum – MAELEZO.
Tume
ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imeendelea kuiasa jamii kuhusu
kubadili tabia ili kuepuka maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwani ugonjwa
huo bado ni janga kwenye nchi yetu.
Hayo
yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa tume hiyo Bw.Jumanne Issango
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu
mafanikio na changamoto za tume tangu ilipoanza kutekeleza majukumu
yake.
“UKIMWI
bado ni changamoto katika maendeleo ya Taifa letu na umeendelea
kuathiri kila sekta, kila imani, matajiri na masikini nchini kote hivyo
ni wajibu wa kila mmoja kujitathmini mwenendo wake na kuacha tabia
hatarishi ambazo zinachangia kuongeza maambukizi ikiwemo uasherati,
ngono zembe, ulevi na kadhalika,” alisema Issango.
Alieleza
kuwa kwa miaka ya karibuni hali ya maambukizi ya UKIMWI imeendelea
kupungua ingawa kuna tofauti kwenye mikoa, wilaya na makundi ya
kijamii.Issango alibainisha kuwa kiwango cha maambukizi Tanzania Bara ni
asilimia 5.3 na takwimu hizo ni kutokana na Utafiti wa Viashiria vya
UKIMWI mwaka 2012.

Kaimu Mkrugenzi Mkuu wa TACAIDS Bw.Jumanne Issango akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa mkutano kuhusu changamoto na mafanikio katika kupambana na virusi vya ukimwi nchini kulia ni Kaimu Mkurugenzi Muitiko wa kitaifa wa TACAIDS Bi.Audrey Njelekela mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za TACAIDS leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Paschal Dotto-MAELEZO)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...