Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
Serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania leo imezindua kituo kipya cha kimarekani kitakachokuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia kakinacholenga kukuza fikra yakinifu na mijadala ya kina kuhusu masuala mbali mbali ya kuwapa wananchi haki ya kupata elimu na kupata taarifa bila kikwazo.
Kituo hicho kitakuwa ni daraja la kuzifikia taasisi za elimu ya juu za Kimarekani, taasisi za utafiti, za kimarekani, na hata ufadhili wa masomo na kushirikisha hulka ya ubunifu na ujasiriamali kwa watanzania watakaobuni mustakabali mpya.” Tunawekeza
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kituo hicho, Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson amesema, kituo hicho kipya kitakuwa kiunganishi cha kidijitali kati ya Tanzania na eneo la Silicon Valley (kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia)Tehama na ubunifu.
Dk.Patterson amesema Vituo vya Kimarekani ni maeneo yaliyotengwa maalumu katika taasisi mbalimbali za nchini Tanzania “kituo hiki cha lugha ya kiingereza tunachofungua leo kitatoa uwezo wa moja kwa moja wa kujifunza lugha ya Kiingerezaa, ushauri wa elimu, na habari kuhusu fursa za elimu Marekani.
Amesema, kituo hiko kilichopo maktaba kuu jijini hapa kitakuwa wazi kutumiwa na wananchi wote bila malipo oyote na kitakuwa wazi kwa umma kwa siku za Jumatatu hadi Ijumaa na jumamosi asubuhi hadi mchana.
Akifungua kituo hicho, Naibu Waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia mhandisi Stella Manyanya amesema, kituo hicho kitakuwa daraja la kuzifikia taasisi za elimu ya juu za kimarekani, taasisi za utafiti na ufadhili wa masomo.
Aidha aliumba ubalozi wa marekani kusaidia kujenga vituo vingine katika mikoa mingi nchini ili kusaidia elimu kwa umma.
Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya pamoja na Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson wakikata utepe kuashiria kufunguliwa kwa kituo cha Kimarekani kilichoanzishwa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania pamoja na serikali ya Tanzania.

Naibu waziri wa Elimu na Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya akihutuba katika uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichoanzishwa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania pamoja na serikali ya Tanzania. Kituo hicho kitakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia kitakachowawezesha wananchi kupata elimu na taarifa bila vikwazo. 

Kaimu balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson akizungumza kuhusu uzinduzi wa kituo cha Kimarekani kilichozinduliwa leo kuwa kitakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu wa teknolojia kitakachowawezesha wananchi kupata elimu na taarifa bila vikwazo.
safi sana
ReplyDelete