Na John Nditi, Ulanga.
KAMPUNI
ya TanzGraphite imesema itawajengea nyumba zenye hadhi ya juu kaya za
kijiji cha Epanko, wilayani Ulanga , mkoani Morogoro zinazohama kwa
kupisha mradi mkubwa wa uchimbaji wa madini ya Kinywe (Graphite) na
itahakikisha kuwa, maisha ya watu wanaohama yanabaki kama ilivyokuwa
awali ikiwa na kuboreshwa zaidi.
Meneja
Mahusiano wa TanzGraphite, Bernard Mihayo , alisema hayo kwenye taarifa
ya Kampuni hiyo katika kikao cha tisa cha kikosi kazi kilichokutana
Septemba 14, mwaka huu mjini Mahenge , wilayani humo.
Kikao
hicho kilichokuwa ni cha kujadili na kupokea mrejesho wa vikao vya
wananchi kuhusu mpango wa uhamishaji makazi (RAP) kupisha mradi wa
madini ya kinywe wa Epanko kilihudhuriwa na wajumbe wa vitongoji vya
Kazimoto, Epanko A, Itatira , Mbera, Epanko B na Luli .
Wawakilishi
wengine ni kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro, Ofisi ya madini
mkoa , Ofisi ya wilaya ya Ulanga , halmashauri na wadau wengine wa
mradi huo.
Madini
ya Graphite ‘Kinywe’ kwa sasa yanahitajika kwa wingi duniani kutokana
na matumizi ya kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo betri za simu ,
kompyuta mpakato ‘laptop’ na penseli .
Kiongozi
wa wa kimila wa kabila la Wapogoro wa kijiji cha Epanko , wilaya ya
Ulanga, mkoani Morogoro (Mbuyi ), Redemta Masura ( wapili kushoto)
akiwa na viongozi wa Kijiji hicho wakipitia taarifa ya mpango wa
uhamishaji makazi kupisha mradi wa madini ya Kinywe wa Epanko , wakati
wa kikao cha tisa cha Kikosi Kazi iliyowashirikiasha wajumbe wa kutoka
vitongozi sita wa kijiji hicho , viongozi kiserikali na kijamii
kilichofanyika hivi karibuni mjini Mahenge.
Baadhi
ya viongozi wa serikali wa wilaya ya Ulanga na mkoa wa Morogoro
wakiungana na vitongoji vya kijiji cha Epanko wakiwemo na wakimila na
kijamii kupitia taarifa ya mpango wa uhamishaji makazi kupisha mradi
wa madini ya Kinywe wa Epanko katika kikao cha tisa cha Kikosi Kazi cha
mpango wa uhamishaji makazi kupisha mradi wa madini ya Kinywe wa
Epanko kilichofanyika hivi karibuni mjini Mahenge.
Baadhi
ya viongozi wa kamati ya Kikosi kazi kutoka serikali za vitongoji vya
kijiji cha Epanko wakiwemo wa kimila na kijamii wilayani Ulanga
wakijumuika na wa ngazi ya wilaya hiyo na mkoa wa Morogoro kupitia
kwa pamoja taarifa ya mpango wa uhamishaji makazi kupisha mradi wa
madini ya Kinywe wa Epanko kilichofanyika hivi karibuni mjini Mahenge.
Katibu
Tawala Msaidizi Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Lucas
Mwaisaka (kulia) akimkabidhi Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Epanko, Kata
ya Nawenge, wilayani Uanga, Eliza Liwemba, ( kushoto) Mpango wa
Uhamishaji Makazi (RAP) wa Mradi wa Madini wa Epanko wakati wa kikao
cha tisa cha Kikosi Kazi cha mpango huo kilichowashirikisha wajumbe wa
kutoka vitongozi sita wa kijiji hicho , viongozi kiserikali ya wilaya
na mkoa ambacho kilifanyika hivi karibuni mjini Mahenge. ( Picha na
John Nditi).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...