Balozi wa
Nordic Foundation Tanzania, Najma Abdallah akiwasiliana na Mwalimu wa Shule ya
Msingi iliyopo Songwe Mkoani Mbeya, Hassan Mwamburi baada ya kuibuka mmoja wa
washindi 10 katika droo ya Pili ya kampeni ya Afyabando iliyofanyika jijini Dar
es Salaam. Washindi watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya zenye thamani ya
shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja na familia.
Balozi wa
Nordic Foundation Tanzania Najma Abdallah akiwasiliana na Diana Peter Mkazi wa
Morogoro baada ya kuibuka mmoja wa washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za Bima ya
afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja na
familia, katika droo ya ya pili ya Afyabando.
Mabalozi wa
Nordic Foundation Tanzania Hilary Daudi' Zembwela' na Najma Abdallah
wakiendesha kampeni ya Afyabando kuwapata washindi 10 watakaokabidhiwa kadi za
Bima ya afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya matibabu pamoja
na familia. Mchezo huo umechezeshwa jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mabalozi wa
Nordic Foundation Tanzania Hilary Daudi' Zembwela' na Najma Abdallah wakiwa na
Mkaguzi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya kubahatisha, Bakari Maggid
aliyesimamia zoezi la kuendesha kampeni ya Afyabando kuwapata washindi 10
watakaokabidhiwa kadi za Bima ya afya zenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa
ajili ya matibabu pamoja na familia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...