Na Binagi Media Group.

Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja mwaka huu 2017, benki ya CRDB jana simetoa semina kwa wateja wake katika wilaya ya Chato mkoani Geita na pia kupokea maoni yao ili kuboresha zaidi huduma zake.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodlack Nkini aliwahakikishia wateja wa benki hiyo huduma ya mikopo kwa muda wa siku saba na hivyo kuwahimiza wafanyabiashara kuitumia benki fursa hiyo kukuza mitaji yao ya biashara.

Aidha alisisitiza kwamba benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake ikiwa ni benki inayoongoza kwa kutoa mikopo hapa nchini huku pia jamii ikiendelea kunufaika na benki hiyo kupitia gawio la faida ambalo hutolewa kila mwaka ili kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo afya na elimu.

“Tunaomba tuendelee kushirikiana pamoja ambapo CRDB ni benki ya muda mrefu iliyo salama na imara kufanya nayo kazi ikiongoza kwa zaidi ya miaka 10 sasa kwa kutoa huduma bora na zenye riba nafuu nchini”. Alisisitiza Nkini kwenye semina hiyo iliyojumuisha pia wateja wa CRDB kutoka Geita, Muleba, Ngara na Bihalamulo.
Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga alisema benki hiyo imeendelea kuwafikia wateja wake kote nchini kupitia huduma mbalimbali ikiwemo Fahari Huduma, Simu Banking pamoja na Internet Banking na hivyo kuwa benki yenye mtandao mkubwa unaowawezesha wateja wake kupata huduma za kibenki popote walipo.

“Huduma zetu ni bora kuliko benki nyingine yoyote nchini hivyo natoa rai wateja wetu kutumia huduma zetu ikiwemo mikopo kwa ajili ya mitaji ya biashara zao kwani tunao uwezo mkubwa wa kuwahudumia”. Alidokeza Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus.
 Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodlack Nkini, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji CRDB. Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus akizungumza kwenye semina hiyo. Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga akizungumza kwenye semina hiyo. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...