Mteja
wa benki ya TIB, Irene Kiwia pamoja na wateja wengine wakishirikiana
kukata keki kwaajili ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo
hufanyika kila mwaka Oktoba.
BENKI
ya biashara inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania Investment Bank
(TIB) inaendelea kutoa huduma mbalimbali za kibenki zenye ubunifu wa
hali ya juu ili kufikia dira ya kuwa benki ambayo ni chaguo la wateja.
Hayo
yamesemwa ka Mkurugenzi mtendaji wa benki ya TIB, Frank Nyabundege
wakati akizungumza na wateja wa benki ya TIB waliofika katika tawi la
Samora jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa benki hiyo inatoa huduma
za TIB mobile, Utoaji wa bure wa dhamana za kibenki, sms alert, Premier
banking, uboreshaji wa kazi za ATM, kutua huduma masaa 24 ya katika tawi
la bandari, huduma za malipo ya kodo kirahisi pamoja na JIPANGE Plan.
Amesema
kuwa "Huu ni mwaka ni waka wetu wa pili tangia kupata kibali cha kutoa
huduma za kibenki na kuendelea kujenga uwezo wa kuwapa wateja huduma za
kipekee."
Amesema kuwa hudum nzuri kwa wateja ndio kipaumbele katika maendeleo ya benki hiyo.
Mteja
wa benki ya TIB, Irene Kiwia akizungumza na Michuzi TV jijini Dar es
Salaam leo wakati alipofika katika benki ya TIB jijini Dar es Salaam
wakati wa kuwashukuru wateja wa benki hiyo.
Mkuu
wa masoko na mahusiano wa Benki ya TIB, Theresia Soka akizungumza na
wateja pamoja na wafanyakazi wa benki ya TIB waliofika katika benki hiyo
jijini Dar es Salaam leo.
Amewashukuru
wateja wa benki hiyo kufka katika taw la Samora kwaajili ya
kusheherekea pamoja wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuwaomba kutoa
maoni yao ili kwenye mapungufu wajirekebisha.
Baadhi
ya wateja na wafanyakazi wa benki ya TIB wakiwa katika hafla fupi ya
kuwashukuru wateja wao katika wiki ya huduma kwa wateja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...