Chama cha Wataalam wa Urembo na Vipodozi Tanzania (CWUVT) wakutana Jijini Dar es salam kwa lengo la kuwakutanisha pamoja wataalamu wa ngozi, wataalamu wa urembo, wataalam wa saluni, wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa za vipodozi. Wanachama waasisi wa chama hicho walikutana chini ya Mwenyekiti Mama Shekha Nasser. Dhira ya Asasi hiyo ni kuinua, kuunganisha na kutumikia sekta ya Urembo na Vipodozi, watabibu wa ngozi na wataalamu wa Saluni ambao huboresha maisha ya watu kila siku. Pia kujenga na kudumisha wanachama ambao uwepo wao ni kukuza na kuunga mkono utaalam katika tasnia ya Urembo na Vipodozi kwa ujumla wake.
Wajumbe waasisi walioudhuria mkutano huo wameipitisha Katiba ya Chama hicho na kuazimia kujitoa na kushirikiana kwa pamoja katika kuelimisha, kuhudumia na kutetea haki za wataalam wa saluni, wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa za vipodozi katika tasnia ya Urembo na Vipodozi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...