Na: Thobias Robert.
Katika kutimiza ndoto ya Tanzania ya uchumi wa kati unaotegemea uzalishaji viwandani, wadau mbalimbali wa maendeleo wamezidi kujitokeza na kutoa mawazo yatakayosaidia kukuza sekta za kiuchumi ili kutimiza ndoto hiyo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza katika Dkt. Samson Kibona, kutoka Antipa Herbal Clinic amesema kuwa uchumi wa viwanda utaokoa kilimo cha Tanzania na kupandishwa thamani ya mazao yalimwayo hapa nchini na kuongeza kipato kwa wakulima wadogo, wa kati na wakubwa.
Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa lengo la kuelezea mbinu za kilimo cha kisasa, kutoa ombi kwa serikali juu ya kusimamia kilimo hicho chenye tija na kitakachopunguza uagizwaji wa bidhaa zitokanazo na kilimo kutoka nje ya nchi.
“Tanzania ya viwanda itaokoa sekta ya kilimo, kupandisha thamani ya mazao na kufanya mazao yanayolimwa nchini kutosafirishwa nje badala yake bidhaa zitokanazo na mazao hayo kama vile mafuta ya kupikia, vyakula vya kawaida, kama biskuti, nafaka halisi ya unga ndizo zitasafirishwa au kuuzwa nje na kuongeza fedha za kigeni,” alieleza Dkt. Kibona.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...