Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mbozi mkoani
Songwe, alipowasili mkoa humo kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye lengo la
kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao na namna
ya kuwasaidia pamoja na kuwakumbusha wajibu wa kutoa huduma bora kwa jamii.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini (IGP) Simon Sirro, akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili
yake alipowasili katika mkoa wa Songwe, kwa ziara ya kikazi ya siku moja yenye
lengo la kuzungumza na maofisa na askari wa Jeshi hilo na kuona changamoto zao
na namna ya kuwasaidia pamoja na kuwakumbusha wajibu wa kutoa huduma bora kwa
jamii.
Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini (IGP) Simon Sirro, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa,
akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo na kupeana
mbinu na mikakati namna ya kukabiliana na matukio ya uhalifu ikiwamo upitishaji
wa magendo kutoka nchi jirani unaofanywa na watu wasiowema. IGP Sirro, yupo
mkoani humo kwa ziara ya kikazi.
Mkuu
wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)
Simon Sirro, wakiwa katika picha na
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo, baada ya kumaliza
kikao kazi cha kupeana mbinu na mikakati namna ya kukabiliana na matukio ya
uhalifu ikiwamo upitishaji wa magendo kutoka nchi jirani unaofanywa na watu
wasiowema. IGP Sirro, yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi. Picha na Jeshi la Polisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...