Na Mwandishi wetu wa Globu ya Jamii.
KATIKA kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo cha hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Chama Cha Mapinduzi(CCM) katibu wa chama wilaya ya ubungo,Salum kali ameweka jiwe la Msingi kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za chama katika tawi la sinza "A"
Akihutubia wanachama walio jitokeza katika shughuli hiyo kali amesema, Baba wa taifa alitengeneza heshima kwa Mtanzania aheshimu kwanza maadili ya taifa lake ndio aweze kuheshimiwa na watu wengine.
aidha kali amesema kuwa , Mwalimu Nyerere aliamini ndani ya chama cha Mapinduzi CCM ndiko kunapo patikana viongozi bora ambao wana uwezo wa kufanya kazi kwa umakini pasipo malumbano wala fujo kama tunavyo ona kwa wenzetu wa pembeni.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Salum Kali akishiriki ujenzi wa ofisi za chama kata ya Sinza A.
Katibu wa chama akizindua jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Sinza "A" Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...