Naibu waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Sinkamba ameziagiza halmashauri zinazodaiwa kwa kutokupeleka michango kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kutathmini kiasi wanachodaiwa na wakati wa maandalizi ya bajeti wahakikishe wanakwenda na mikakati ya kiasi walicholipa wanachodaiwa na namna ya kulipa madai kwenye mifuko hiyo.
Agizo hilo limetolewa leo wakati Bw Sinkamba akizindua ofisi za mfuko wa penisheni wa LAPF kanda ya magharibi ambayo itahudumia Mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita na Wilaya ya Sengerema na Halmashauri ya Buchosa.
Amesema miongoni mwa maeneo yanayodaiwa na mifuko ya hifadhi ni pamoja na watumishi wa Halmashauri hususani watendaji wa kata na vijiji na kwamba ni vema Halmashauri zikajua kiasi wanachodaiwa na kuandaa mikakati ya kulipa na kupeleka taarifa ya malipo kwa TAMISEMI.
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw Eliud Sanga, ameeleza katika kuendelea kuboresha huduma ya mfuko huo wamekuwa wakilipa mafao mapema zaidi kwa mwanachama anayekaribia kustaafu na kwamba wamejidhatiti kutoa huduma bila usumbufu kwa wastaafu wanapohitaji mafao yao.Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amesema wanaamini kwa mashirika kuendelea kuweka ofisi za kanda ni njia mojawapo ya kukuza mji wa Geita na kufikia azma ya kuufanya mji huo kuwa Manispaa.
Naibu waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Josephat Sinkamba Akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Kushoto Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,Kulia Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw Eliud na wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Geita Mji Constatine Kanyasu wakikata utepe kwaajili ya kuzindua ofisi za LAPF kanda magharibi .
Philip Ngika ni Mstaafu aliyestaafu hivi karibuni na kupatiwa mafao yake kiasi cha zaidi ya Milioni 72 na Naibu waziri wa TAMISEMI.
Mwanachama wa LAPF ambaye amenufaika na fao la uzazi na kupatiwa kiasi cha zaidi ya Shilingi Laki sita
Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Bw Eliud Sanga,Akimkabidhi Mgeni rasmi Naibu waziri wa TAMISEMI madawati 100 ambayo yametolewa kwenye halmashauri ya mji wa Geita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...