Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) anawatangazia wahitimu na wadau wote wa DIT kuwa Mahafali ya Kumi na Moja (11) ya Taasisi yamepangwa kufanyika Jumamosi, tarehe 16 Desemba, 2017.

Mahafali haya yatatanguliwa na siku ya utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao katika mwaka wa masomo 2016/2017, sherehe ambazo zitafanyika Ijumaa, tarehe 15 Desemba, 2017.

Taasisi inapenda kuwataarifu wahitimu wa Shahada ya Uzamili (M.Eng) na Shahada ya Kwanza (B.Eng/BTech), kusoma utaratibu na hatimaye kuthibitisha ushiriki wao katika  Mahafali hayo kupitia tovuti ya Taasisi (www.dit.ac.tz)

Wahitimu watakaoshiriki wanapaswa kulipia joho la Mahafali Tsh. 50,000/= (kwa wahitimu wa Shahada ya Uzamili) na Tsh. 30,000/= (kwa wahitimu wa Shahada ya Kwanza katika tawi lolote la NBC kwenye akaunti namba 018101003145 na hatimaye kujisajili kupitia tovuti ya Taasisi www.dit.ac.tz)Watakaoruhusiwa kushiriki Mahafali haya ni wale tu watakaokamilisha usajili wao.

ZINGATIA: Malipo yafanyike kwa kutumia jina kamili kama linavyoonekana kwenye orodha ya wahitimu wa mwaka 2016/17 iliyopo kwenye tovuti ya Taasisi, namba ya usajili na madhumuni ya malipo yaani Mahafali.

Kwa wanafunzi wa Stashahada (OD) ambao hawatavaa majoho wanatakiwa kuvaa nguo safi, nadhifu na zenye staha.  Na hawa wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kupitia tovuti ya  Taasisi (www.dit.ac.tz) bila kulipia gharama zozote.

“Rehersal” itafanyika Alhamisi, tarehe 14 Desemba, 2017.

Mwisho wa kujisajili ni tarehe 15 Novemba, 2017.

Atakayeona tangazo hili anaombwa kumjulisha mwenzake.

Tangazo hili limetolewa na:

Ofisi ya Uhusiano,
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam,
S.L.P 2958,

Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...