Kabati aliliomba jeshi la polisi mkoani Iringa kuhakikisha wanapeleka dawati la jinsia katika shule za msingi na sekondari ili kupunguza na kumaliza kabisa tatizo la ubakaji kwa wanafunzi kwa kuwa watakuwa wazi kuzungumza wanachofanyiwa huko mitaani. Mbunge huyo alichangia kiasi cha sh. milioni moja kwa ajili ya kusaidia dawati hilo.
Kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi na mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakicheza ngoma wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF).
Hawa ni baadhi ya wanamtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) wakiwa katika maadhimisho ya miaka kumi toka kuanzishwa kwa mwaka 2007.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...