Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya kesi yake iliyokuwa ikimkabili ya matumizi ya dawa za kukevya aina ya heroine. Mshtakiwa Manji ameachiwa chini ya kifungu cha sheria Namba 235 cha mwenendo wa makosa ya jinai.
Hukumu hiyo imesomwa leo mchana na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambaye amesema ni wajibu wa upande wa mashtaka kuthibitisha makosa kwa mshtakiwa bila ya kuacha shaka.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha amesema, kuna baadhi ya kesi zinahitaji zaidi utaalamu kutoka kwenye fizikia na madawa zaidi ya sheria. Amesema kwa utetezi ulivyotolewa unaonyesha kuwa polisi walimsaidia mshtakiwa kupata dawa zake alipokuwa kituoni na hata gerezani.
Manji ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika orodha ya watu wanaodaiwa kujihusisha na kutumia dawa za kulevya February 6 mwaka huu na kuwataka walipoti kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO).
Awali kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo, upande wa mashtaka ulisema ungeleta mashahidi kumi lakini wakaishia kuleta watatu na Manji alisema angeleta mashahidi kumi na tano lakini walileta mashahidi saba tu ambao kupitia hoja za pande zote mbili mahakama imejiridhisha pasi na shaka ya kwamba mshtakiwa huyo hana hatia baada ya upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha kosa lake.
Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa shtaka lake.
Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa hukumu na kujulikana kuwa upande wa mashtaka hawakuweza kuthibitisha kama kweli alikuwa anatumia dawa za kulevya.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa hukumu na kujulikana kuwa upande wa mashtaka hawakuweza kuthibitisha kama kweli alikuwa anatumia dawa za kulevya.
.
Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akielekea kwenye gari kwaajili ya kuondoka huku akiwa hana kosa mara baada ya kusomewa hukumu na kuonekana kuwa hakuwa akitumia dawa za kulevya.
Mfanyabiashara maarufu,Yusuf Manji aliyekuwa anakabiliwa na matumizi ya Dawa za Kulevya akipanda gari akipanda gari mara baada ya kusomewa hukumu ya kesi iliyokuwa ikimkabiri ya kutumia dawa za kulevya ikiwa upande wa mastaka walishindwa kuthibitisha shtaka hilo.
Wakili wa Manji Bi. Hajra Mungula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya mteja wake kuonekana hana kosa la matumizi ya dawa za kulevya.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...