Na Mathias canal, Singida

Wajumbe wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida  Vijijini Mkoani Singida wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wa ngazi mbalimbali za Wilaya, wawakilishi wa ngazi ya mkoa na Taifa.

Mkutano huo ulifanyika katika Kijiji na Kata ya Ilongelo na kuhudhuruwa na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM Wilaya kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM.

Mwenyekiti mpya wa CCM Wilaya ya Manyoni aliyechaguliwa kwa kura za kishindo ni William Mwang'ima Nyalandu aliyepata kura 440, akifatiwa na FATUMA Ihonde aliyepata kura 189 na nafasi ya tatu ilikamatwa na Alex Mdidi Lissu aliyepata kura 159.

Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika alisema kuwa uchaguzi huo umekamilika kwa amani na salama kwa kufuata taratibu na kanuni za uchaguzi zilizoelekezwa na Chama Cha Mapinduzi.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini Bi Grace Shindika akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Singida Vijijini ikijihuzuru mbele ya wajumbe muda mchache kabla ya mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Singida Vijijini akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Singida Vijijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...