NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka wakulima na wafugaji wa vijiji vinne alivyotembelea vya wilaya ya Mkuranga kuondokana na tofauti zao na badala yake wapendane.
Hayo aliyasema katika ziara yake kwa wananchi wa jimbo lake la Mkuranga-Pwani ambapo aliweza kuelezwa kero mbalimbali na kuahidi kuzishughulikia.
Katika ziara hiyo pia aliweza kuchangia jumla ya fedha kiasi cha shilingi Mil.6 pamoja na mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati zilizomo katika vijiji hivyo.
Aidha pia amewaomba wananchi kuunda vikundi mbalimbali vya ujasiriamali hususani ufugaji wa kuku samaki na mifungo mbalimbali ili kuwawezesha kuondokana na umaskini.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega ambaye ni Mbunge wa Mkuranga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyanduturu akiwa ni ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake kuwa Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiangalia ujenzi wa jengo la zahanati ya kijiji cha Nyanduturu kata ya Nyamato ambayo pia amechangia Millioni moja na nusu pamoja na saruji 50 ili kufanikisha ujenzi huo unaoendelea.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mvuleni,Mohammed Mpunjika akimkabidhi risala yao Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega alipofanya ziara yake ya kwanza tokea kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Mmoja wa akina mama kutoka katika kijiji cha Tipo kata ya Nyamato akiuliza swali kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wakati alipofanya ziara yake .
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga,Ally Mohammed akizungumza jambo.
Muonekano wa jengo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...