Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wametoa pongezi kwa Mfuko wa Pensheni wa PPF
kwa kutoa huduma bora zinazoendana na viwango vya kimataifa .
Wakizungumza hii leo katika kilele cha wiki ya huduma kwa wateja, baadhi ya wateja waliofika
ofisini hapo kupata huduma mbalimbali wamesema weledi na uharaka wa kupata huduma toka
kwa wafanyakazi wa Mfuko huo ni jambo la kuigwa na taasisi nyingine nchini.
Jessica Mmasy ni miongoni mwa wanachama waliofika kupata huduma hii amesema upotevu wa
muda wa kungoja huduma katika ofisi mbalimbali imekuwa kikwazo kikubwa nchini lakini PPF
wamepata suluhisho la changamoto hiyo.
“Nimehudumiwa ndani ya dakika tano tu, kitu ambacho ni sehemu chache unaweza kukuta hivyo
wanatoa huduma kwa makini wapo ‘professional’(weledi) na wanajali muda wa mteja,”
amesema mteja huyo ambae alifika ofisini hapo kupata huduma.
Naye Mustafa Adamu ambaye ni mwanachama wa PPF amesema mfumo wa utoaji huduma
katika ofisi za PPF unatoa nafasi kwa kila mwanachama kuhudumiwa kwa usawa na bila
manungĂșniko.
“Hapa ukifika wa kwanza,utakuwa wa kwanza kuondoka pia,kuna mfumo maalumu wa
kuhudumiwa kutokana na namba unayopewa hivyo hakuna kugombania kwenda kwenye dirisha
la mhudumu,” alifafanua mteja huyo.
Kwa upande wake meneja wa huduma kwa wateja wa Mfuko huo Michael Christina amesema
wameienzi wiki ya huduma kwa wateja kama sehemu ya utendaji wao wa kazi wa kila siku.
“Tumepata cheti cha kutoa huduma kwa kiwango cha kimataifa (ISO 900: 2015 certified) hivyo
kutoa huduma bora ni jadi yetu kila siku katika utekelezaji wa majukumu yetu”,amesema meneja
huyo.
Meneja Uhusianao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Lulu Mengele (kushoto) akimwelezea huduma
zinatolewa na Mfuko huo mwanachama wa PPF Mustafa Adamu (kulia) alipofika katika ofisi za Mfuko
huo kupata huduma.
Mwanachama wa PPF Wiliam Dagharo (Kushoto) akisisitiza jambo kwa mtoa huduma wa PPF katika
ofisi za Mfuko wa PPF Makao Makuu jijini Dar es Salaam hii leo.
Mwanachama wa Mfuko wa PPF Bi.Mkemwema Said (kulia) akipata huduma katika ofisi za PPF jijini
Dar es Salaam hii leo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja duniani.
Meneja wa huduma kwa wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Michael Christian (Kushoto) akitoa
huduma kwa mwanachama wa PPF Jessica Mmasy (kulia) aliyefika katika ofisi za PPF Makao Makuu jijini
Dar es Salaam tarehe 6/10/2017 katika kilele cha wiki ya huduma wateja.
Wateja mbalimbali wakipata huduma katika ofisi za Mfuko wa Pensheni za PPF hii leo jijini Dar es
Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...