Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 53 cha
Katiba ya Zanzibar ya 1984 na Kifungu 12 (3) cha Sheria ya
Utumishi wa Umma Namba 2 ya mwaka 2011, Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali
Mohamed Shein, amefuta uteuzi wa MKURUGENZI MKUU WA
SHIRIKA LA NYUMBA NDUGU MOHAMMED HAFIDH RAJAB
kuanzia leo tarehe 12 Oktoba, 2017.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na
Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO
ZANZIBAR
12 OKTOBA, 2017
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...