MAREHEMU HARRIS CHARLES MWAKITOSI
(1941 - 2017)
Familia ya Marehemu Harris Charles Mwakitosi
wa Changanyikeni kwa moyo mkunjufu, tunapenda kuchukua nafasi hii kutoa
shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, majirani na marafiki kwa msaada wa hali,
mali na faraja walioutoa kwa familia katika kufanikisha shughuli zote za msiba
wa Baba yetu mpendwa Mzee Harris Charles Mwakitosi aliyefariki ghafla tarehe 29
Agosti, 2017 Dar es Salaam na kuzikwa Kijijini kwao Mseke – Iringa tarehe 02
Septemba, 2017. Marehemu Harris
Charles Mwakitosi alikuwa Mume wa Bi. Juliana M.E Mwakitosi na Baba wa Laura,
Lina, Lilian na Arthur. Pia alikuwa Mkwe wa Gratian, Andrew na Upendo.
Kwa namna ya pekee familia inapenda
kutoa shukrani za dhati kwa Uongozi na Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge, Uongozi
na Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na
Mawasiliano, Fr. Mvungi - Paroko wa Parokia ya Utatu Mtakatifu - Changanyikeni,
Fr. Ngowi, Fr. Eugen Mwanyika, Jumuiya ya Mtakatifu Thomas – Changanyikeni, Majirani
– Changanyikeni, Vikundi mbalimbali (social
groups) vya marafiki wa watoto wa marehemu, Wana Mseke, Wana Uwemba na Wana
Kantare. Asanteni sana kwa sala, maombi, misaada ya hali na mali na kujitokeza
kwenu katika kutufariji na kututia nguvu wakati wa majonzi.
Aidha, tunapenda kutoa shukrani nyingi
kwa majirani, ndugu, jamaa na marafiki kwa misaaada yenu ya hali na mali na pia
kushiriki katika shughuli zote za msiba na mazishi. Shukrani kwa wote mliofika
nyumbani, mliotupigia simu au kutuma ujumbe kwa njia mbalimbali kwa lengo la
kutufariji na kututia nguvu, tumefarijika sana. Tunawashukuru kwa kutuonyesha
upendo wa dhati katika kipindi hiki kigumu kwetu. Ni dhahiri msiba huu haukuwa
wetu peke yetu, ulikuwa wetu sote.
Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mmoja
peke yake, tunaomba mpokee shukrani hizi wote mliohusika kwa namna moja ama
nyingine katika kufanikisha shughuli yote ya msiba wa Baba yetu Mpendwa Charles
Mwakitosi. Hatuna cha kuwalipa na itoshe kusema ASANTENI SANA na Mwenyezi Mungu awajalie na kuwazidishia mahitaji
yenu ya kila siku.
Familia inapenda kuwaalika nyote
kwenye Ibada ya Shukrani ya Siku Arobaini (40) tangu kifo chake itakayofanyika
katika Kanisa la Parokia ya Utatu Mtakatifu – Changanyikeni Siku ya Jumapili
tarehe 08 Oktoba 2017 kuanzia saa 2:00 Asubuhi na baadaye kwenye chakula cha
Mchana Nyumbani kwa Marehemu Changanyikeni kuanzia saa 7:00 Mchana.
2
Timotheo 4:7 “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani Nimeilinda” Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga
wa Milele umuangazie, apumzike
kwa amani Amina.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...