Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, akitoa somo kwa wajasiriamali juu ya umuhimu wa kujiunga na kujiwekea akiba kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa manufaa ya sasa na baadaye ya familia, wakati wa Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Wajasiriamali wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika (hayupo pichani) katika Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Afisa Uhusiano wa Mamaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Agnes Lubuva (kulia), akigawa vipeperushi vya taasisi hiyo, kwa wajasiriamali waliohudhuria kongamano hilo la Wiki ya Fursa za Kifedha na Uwekezaji, viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde Msika, akijibu maswali ya wajasiriamali katika kongamano hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...