Mkurugenzi
wa Marie Stopes Eng Anil Tambay akielezea namna walivyoweza kutoa
huduma ya upimaji wa saratani ya mlango wa shimgo ya kizazi kwa wanawake
nchini wakiwa wameweza kupima jumla ya wanawake 187,267 na asilimia
4.2 sawa na wanawake 7,783 wakikutwa tayari wana mabadiliko ya awali ya
dalili za saratani ya mlango wa kizazi kwa kipindi cha miaka mitano
waliyofanya kazi sambamba na Shirika la PSI Tanzania na Chama cha Uzazi
na Malezi (UMATI)
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SERIKALI imenunu vifaa tiba 100, vya tiba mgando ya mabadiliko ya awali ya
saratani ya mlango wa shingo ya kizazi (cryotheraapy) huku Tanzania ikiwa kinara wa
ugonjwa huo Afrika.
Hayo yalibainishwa leo wakati wa kufungwa kwa mradi wa uchunguzi na
matibabu ya awali ya saratani ya mlango wa shingo ya kizazi uliofanyika miaka
mitano kwa ushirikiano wa Chama cha Wazazi na walezi(UMATI), PSI na Marie Stopes kwa uwezeshwaji wa taasisi ya Bill and Gates.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mama na Mtoto
kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk Safina
Yuna, amesema mradi huo umesaidia kuboresha upatikanaji wa mabadiliko ya
saratani ya mlango wa shingo ya kizazi katika vituo 90.
"Kama mnavyojua Tanzania inaongoza kwa saratani ya mlango wa kizazi hawa
wametusaidia, Serikali imeamua kupanua wigo na kupunguza gharama za
matibabu kwa wagonjwa."amesema.
Amesema takwimu zinaonesha kuwa wagonjwa wengi hufika hospitali ya Ocean
road wakiwa katika hatua za mwisho ambapo matokeo ya matibabu yanakuwa
si mazuri huku akibainisha mgonjwa akiwahi hupona.
Amesema vifaa tiba hivyo vitatumika kutibu matibabu ya awali na upasuaji
mdogo kwa wagonjwa wenye mabadiliko makubwa ambapo tayari
vimeshasambazwa katika vituo 466 hapa nchini .
"Tutatanua zaidi kuhakikisha huduma hizi zinawafikia walengwa wengi ambao
hawawezi kufika katika hospitali za wilaya na Mikoa pamoja na vituo vya afya
nchini."
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mifumo ya Afya ya Marie Stopes, Jeremia
Makula amesema mradi huo umefika katika mikoa 22 nchi nzima katika vituo
61 vilivyokuwa vikitoa huduma.
"Katika kipindi cha maiaka 5 tuliwafikia wanawake 187,267 katika uchunguzi
wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi na tumegundua asilimia 4.2
walikuwa na mabadiliko ya awali ya kansa ya kizazi,"amesema.
Ameongeza kuwa wametibu wanawake 7600 sawa na asilimia 100 ya
waliokuwa wakihitaji matibabu ya awali ya mabadiliko ya awali ya saratani ya
mlango wa shingo ya kizazi.
Amesema wanawake 1000 wamekuwa wakihitaji huduma ya juu huduma
ambapo walipewa rufaa ya matibabu katika hospitali zinazotoa huduma hiyo.
Makula amesema katika mradi huo wameanza kutumia kipimo kipya ambacho
hakijawahi kutumika hapa nchini licha ya kuwa na changamoto nyingi katika
kuwafikia waliokuwa vijijini.
Mkurugenzi
wa masuala ya uzazi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Safina Yuna akizungumza namna seriakali walivyoweza
kuongeza vituo na kufikia 436 nchi nzima na kuongeza vifaa tiba 100 kwa
ajili ya matibabu ya awali katika hospitali za Wilaya na Mkoa na juhudi
hizo ni katika kupunguza ongezeko la saratani ya mlango wa shingo ya
kizazi kwa wanawake nchini.
Dr
Mary Rose Kahwa Giattas kutoka shirika la JHPIEGO linalojishughulisha
na masuala ya udhibiti wa saratani ya kizazi wakishirikiana na serikali
akitoa pongezi kwa Shirika la PSI Tanzania , Chama cha Uzazi na Malezi
(UMATI) na Marie Stopes kwa juhudi kubwa walizozifanya kwa kutoa huduma
ya upimaji wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi kwa wanawake kwa
kipindi cha miaka mitano, Kulia ni Mshauri wa masuala ya udhibiti wa wa
kansa ya kizazi Dr. Robert Kamala na kushoto ni mratibu wa masuala ya
udhibiti wa wa kansa ya kizazi Dr. Edwin Swai.
Mkurugenzi
wa Afya ya Uzazi kutoka Shirika la PSI Tanzania Prudence Masako
akizungumza nama walivyoshirikiana na Chama cha Uzazi na Malezi (UMATI)
pamoja na Marie Stopes katika kuwasaidia wanawake wenye matatizo ya
saratan ya mlango wa shingo ya kizazi sambamba na changamoto
walizokutana nazo kwenye miaka mitano ya mradi wao ambapo wanawake wengi
wameshindwa kupata huduma zinazostahiki kutokana na kukosa fedha za
matibabu,pia kwenye vituo vyao takribani 22 wamekuwa wanahudumia
wanawake wasiozidi 20 kwa mwezi mmoja.
Dr
Lugano Daimon kutoka Chama cha Uzazi na Malezi (UMATI) akielezea namna
walivyoweza kushirikiana na Shirika la PSI Tanzania na Marie Stopes
katika kutoa huduma ya upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi kwa miaka
mitano na kupitia vituo vyao 11vilivyopo nchini wamepima jumla ya
81,802 na katika hao jumla ya wanawake 2,862 sawa na asilimia 3.5
wakutwa tayari wana viashiria vya saratano ya mlango wa shingo ya
kizazi.
Baadhi
wa washiriki kutoka sehemu mbalimbali wakiwa wanafuatilia mkutan huo wa
ufungwaji wa mradi wa miaka mitano wa kutoa huduma ya kupima saratani
ya mlango wa kizazi kwa wanawake nchini uliokuwa chini ya Shirika la
PSI Tanzania, Chama cha Uzazi na Malezi (UMATI) na Marie Stopes.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...