WAFANYAKAZI wa bima ya Britam ambayo hutoa bima za magari, bima za nyumba, bima za wakandarasi, bima za usafiri wa majini pamoja na bima za safari bima za afya pamoja na nyingine nyingi leo wametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi hao wametoa vitu mbalimbali kama vile Unga kilo 300
Maharage 250,Sukari kilo 200,sabuni za unga,Karatasi nyeupe (limu bunda)200,Daftari boksi 500, Mafuta ya kula lita 100,chumvi pamoja na vifaa mbalimbali vya shule.
Vitu hivyo vyote vimegharimu shilingi milioni Saba ambayo wameona wagawane faida waliyoipata katika kushaherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba duniani kote.
Kwa upandewa Katibu mtendaji wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA, Hasan Khamis amewashukuru uongozi kampuni ya bima ya Britam kwa kuwaona wao kwani kunavituo vingi hapa nchini "Tunashukuru kwa kutuona sisi CHAKUWAMA na kwa kuona mchango wetu.
Mkuu wa operesheni wa Bima ya Britam, Farai Dogo akimkabidhi msaada wa vitu mbalimbali Katibu Mtendaji wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA, Hasan Khamis kilichopo Sinza jijinini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza Oktoba duniani Kote.

Wafanyakazi wa bima ya Britam wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakikabidhi vitu mbalimbali kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo sinza jijini Dar es Salaam. 

Katibu mtendaji wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWA, Hasan Khamis akizungumza na wafanyakazi wa bima ya Britam na kuwaelezea historia ya kituo hicho pamoja na changamaoto pamoja na mafanikio waliyoyapata.
Baadhi ya wafanyakazi wa bima ya Britam wakimsikili katibu Mtendaji wa kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Bima ya Britam wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...