Mapema leo Ijumaa Oktoba 13,washiriki hao wa shindano hilo la mrembo wa mkoa wa Shinyanga linalotarajiwa kufanyika Oktoba 15 mwaka huu,walimwagilia maji miti mbalimbali iliyopandwa mjini Shinyanga.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo,Mwandaaji wa shindano la Miss Shinyanga mwaka 2017,Grace Shija alisema pamoja na kufanya maandalizi ya shindano hilo pia wanashiriki katika shughuli za kijamii.
“Sisi kama sehemu ya jamii tumeamua kushiriki katika kampeni ya upandaji miti kwa kumwagilia maji miti iliyopandwa katika maeneo mbalimbali mjini Shinyanga kwa kujaza maji kwenye chupa zilizowekwa kutiririsha matone ya maji kwenye miti hiyo”,alieleza Shija.
Akizungumzia kuhusu shindano la Miss Shinyanga mwaka huu alisema jumla ya warembo 12 kutoka wilaya zote za mkoa wa Shinyanga watachuana siku ya Jumapili Oktoba 15,2017 katika ukumbi wa NSSF ya Zamani mjini Shinyanga kuanzia saa mbili usiku ili kupata mrembo wa mkoa mwaka huu.
Washiriki wa shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga “Miss Shinyanga 2017”,wameunga mkono kampeni ya upandaji miti iliyoanzishwa katika wilaya ya Shinyanga na Mkuu wa wilaya hiyo Josephine Matiro hivi karibuni ili kupambana na hali ya ukame/jangwa mkoani humo.
Washiriki wa shindano la kutafuta mrembo wa mkoa wa Shinyanga “Miss Shinyanga 2017” wakiwa wamebeba madumu ya maji kwa ajili ya kuweka kwenye miti ambayo inamwagiliwa maji kwa njia ya makopo ya maji yaliyotobolewa kwa ajili ya kutoa matone kidogo kidogo
Zoezi la kumwagilia maji miti likiendelea
Warembo wakielekea katika eneo jingine kwa ajili ya kumwagili maji miti iliyopandwa hivi karibuni
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...