Naibu mkuu program ya Engine na kiongozi wa kitengo cha Mitaji na Ustawishaji, Scott Bennett (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari  wakati wa uzinduzi wa Mradi jukwaa la kidigitali la Bizfundi kwa ajili ya kutoa usaidizi kwa wajasiliamali na wafanyabiashara ndogondogo kwa kuwaunganisha na wakufunzi na wataalamu wa masuala ya biashara kutambua haki zao.  Pembeni kushoto ni mratibu wa ushirikiano wa taasisi hiyo,  Immaculate Mwaungulu na kushoto ni Canisius Mwita.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mradi wa kuwezesha ukuaji kupitia uwekezaji wa biashara (Engine) chini ya ufadhili wa shirika la  Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), leo imezindua jukwaa la kidigitali la Bizfundi kwa ajili ya kutoa usaidizi kwa wajasiliamali na wafanyabiashara ndogondogo kwa kuwaunganisha na wakufunzi na wataalamu wa masuala ya biashara kutambua haki zao. 

Jukwaa hilo lina lengo la kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi na hatimaye kufanikisha kuwa na ukuaji wa uchumi ambao ni shirikishi na wenye wigo mpana kwenye mikoa ya Sagcotya Mbeya, Iringa, Morogoro na Zanzibar.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Naibu mkuu program ya Engine na kiongozi wa kitengo cha Mitaji na Ustawishaji, Scott Bennett, amesema, Bizfundi itakuwa ni nyenzo ya kuzikutanisha biashara ndogondogo na za kati pamoja na wataalamu wa kutoa ushauri wa biashara  na kutambua soko lao na kusaidiwa kuboresha utendaji na kukuza biashara zao.

“Jukwaa hilo la kidigitali ambalo linapatikana pia kwenye mtandao, litawawezesha wafanyabiashara ndogo ndogo kupata taarifa, usaidizi na mitaji inayohitajika  wakati wa kutoa huduma za ushauri wa biashara na mashirika ya kifedha pia yataweza kunufaika na mtandao mkubwa zaidi wa wateja kwani mpaka sasa, jukwaa lina wamiliki wa bishara na watoa huduma za ushauri wapatao 200 waliojisajili,ammesema Bennet.

Amesema mpaka sasa Bizfundi imesajili wamiliki wa biashara zaidi ya 130,idadi ambayo inatarajiwa kupanda kutokana na muingiliano kati ya biashara ndogondogo na watoa huduma za ushauri wa biasharana kuongeza , kwa sasa Engine inashughulikia uundwaji wa huduma ya kuwaandaa wakopaji  kitu kitakachosaidia wafanyabiashara ndogo ndogo kupata mikopo kwa shughuli zao.

Naye,mkuu wa kitengo hicho, Goodluck Mosha, amesema, jukwaa la Bizfundi litaleta ustawi na uwezo wa soko endelevu kwa watoa huduma za ushauri wa biashara kwa kuhakikisha wafanyabiashara ndogo ndogo na zile za kati zinaweza kupata kwa urahisi usaidizi wa kuimarisha biasharazao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...