Na Agness Francis, Blogu ya jamii.
Mtandao wa Policy Forum( PF) ambao umetimiza miaka 9 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2008 ambapo ilianza kutumia  dhana ya  ufuatiliaji wa uwajibikaji  jamii ( Social Accountability Monitoring) wameungana na wadau katika mkutano wa kujadiliana mafanikio, changamoto  pamoja na mafunzo kutoka kwa wadau mbalimbali wanaotumi dhana hiyo hapa nchini.

Akizungumza hayo leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere Kaimu mwenyekiti  Mtandao wa Policy Forum  ( PF), Herbon Mwakagenda amesema kuwa lengo hasa la mkutano huo ni  kuboresha mbinu zinazotumika na wadau  pamoja na kuangalia mafunzo ambayo yanaweza kutumika kwa ujumla ikiwemo pia kutoa pongezi kwa wananchi  kwa kuwa na muamko mkubwa wa kufatilia  haki zao katika mashirika mbalimbali ya Umma. 
Nae pia  Mratibu wa mtandao wa Policy Forum  (PF), Bw. Semkae Kilonzo amezungumzia lengo kuwa  ni kutaka  kubadiilishana uzoefu na taasisi mbalimbali ili kuweza kuboresha zaidi   uchechemuzi  wa kutekeleza miradi  yao hapa nchini.
Vile vile Mwenyekiti  Mwakagenda aliongezea hasa kwa kuzungumzi a changamoto zinazo wakabili wakati wa kufikisha ujumbe kwenye Halmashauri  mbalimbali  kutokana na ubadilishwaji wa viongozi wa halmashauri hizo na kusababisha taarifa kuchelewe kufika kama inavyotakiwa.
Diwani Kiteto Manyara,Paulo Tunyon ametoa pongezi za dhati kwa wadau wa  mtandao wa Policy Forum( PF) kwa kuweza kupeleka mabadiliko  Vijijini kwa kukabiliana na changamoto hizo kutokana na uwelewa mdogo wa wananchi hao..
Mratibu wa mtandao wa Policy Forum ( PF), Bw. Semkae Kilonzo  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna watakavyoweza kukabiliana na changamoto  ili kufikia malengo ya juu zaidi wanayokusudia leo Jijini Dar Es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere 
  Kaimu mwenyekiti  Mtandao wa Policy Forum( PF), Bw. Herbon Mwakagenda  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mtandao huo jinsi unavyofanya kazi na wadau wa Taasisi mbalimbali hapa nchini leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere.
Wadau wa kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini waliojitokeza kuhudhuria mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...