Na Lorietha Laurence-WHUSM,Dodoma

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amemshukuru Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi. Wang Ke kwa kuipatia wizara vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi milioni 133.

Waziri Dkt. Mwakyembe ametoa shukrani hiyo leo Ofisini kwake Mkoani Dodoma alipokutana na Balozi huyo ambapo waliweka sahihi ya makabidhiano ya vifaa hivyo na kuhaidi kuendelea kuimarisha uhusiano huo uliodumu kwa muda mrefu .

“Nashukuru sana Balozi kwa kutupatia msaada wa vitendea kazi na tunaahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili kwa manufaa ya taifa na watu wake” amesema Mhe.Dkt. Mwakyembe.

Aidha Waziri Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa tayari kumekuwa na juhudi za wazi zinafofanywa na Ubalozi huo kwa kutoa mafunzo ya kubadilishana utaalam kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa china kupitia sekta za filamu, habari,michezo na utamaduni.

Pia, Dkt. Mwakyembe alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania imepata nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika wenye lengo ya kuhifadhi kumbukumbu za harakati za kuikomboa Afrika ili kuwa na historia nzuri kwa kizazi kijacho.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi. Wang Ke (Kulia) katika ofisi za Wizara leo Mkoani Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi. Wang Ke (Kulia) wakiweka saini makubaliano ya kukabidhiana vifaa vya ofisi vyenye thamani ya shilingi milioni 133 katika ofisi za Wizara leo Mkoani  Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi. Wang Ke (wa pili kulia) pamoja na watendaji wa Wizara leo Mkoani Dodoma.Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,DODOMA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...