Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeupongeza mfuko wa Abbott kutokana na juhudi kubwa za kusaidia kuboresha huduma ya afya katika sekta ya afya nchini.

Kauli hiyo imetolewa Leo na Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu kabla ya kukabidhi kadi za bima ya afya kwa watoto 139 wanaoishi katika mazingira magumu.Mfuko huo kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na benki ya ABC, leo wamekabidhi kadi kwa watoto hao kupitia Waziri Ummy Mwalimu.

“Napenda kuupongeza Mfuko wa Abbott kwa kuwezesha watoto hawa 139 kupata kadi za bima ya afya, hongereni sana. Nimeambiwa Kadi hizi mmezilipia na zitaisha baada ya mwaka mmoja, hivyo naomba muendelee kuzilipa endapo haitawezekana Serikali italipa, lakini naamini kwamba hamtashindwa kuendelea kuiunga mkono Serikali,” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Baada ya Waziri huyo kutoa kauli hiyo, Mkurugenzi wa Miradi endelevu wa Mfuko wa Abbott, Dkt. Festo Kayandabila alisema kuwa wako tayari kuwasaidia watoto hao.Mfuko wa Abbott umekuwa ukiisaidia Hospitali ya Taifa Muhimbili katika juhudi zake za kuboresha huduma za afya. Mfuko huo umesaidia kukarabati Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali pamoja na kukarabati Jengo la maabara kuu.
Mkurugenzi wa Miradi Endelevu wa Mfuko wa Abbott, Dkt. Festo Kayandabila akieleza jinsi mfuko wa Abbott ulivyoshiriki kuwapatia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kadi za bima ya afya. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati wa benki ya ABC, Joyce Malai na Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Kurasini, Rabikira Mushi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...