Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ameshauri Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) uanzishe kazi za ajira za muda, kwa walengwa wa Mpango huo kutoka jamii ya Wahadzabe waliopo Wilayani Mkalama ili uwasaidie kuinua uchumi wao.
Dkt Nchimbi ametoa ushauri huo mara baada ya kutembela kijiji cha Singa Wilayani Mkalama na kuona bwawa litakalotumika kuhifandhi maji ya mvua kwa ajili ya shughuli mbalimbali lililojengwa na walengwa wa Tasaf Kijijini hapo kisha kutembelea kijiji cha Munguli Kata ya Mwangeza Wilayani humo aliposhuhudia malipo ya walengwa wa kihadzabe wa Mpango wa Tasaf.
Ameeleza kuwa jamii ya wahadzabe hawana mradi unaohusisha kazi za ajira za muda ambazo zimekuwa zikisaidia katika kuongeza kipato, kuwafundisha thamani ya kazi pamoja na kutekeleza miradi ambayo imekuwa ikisaidia jamii nzima kama vile mabwawa na barabara.
“Nashauri TASAF kabla ya msimu huu wa mvua kuisha muwaletee na hawa wahadzabe mradi wa ajira za muda kama ambavyo walengwa wa vijiji vingine wamekuwa wakifanya kazi hizo na zimekuwa zikichangia maendeleo kwa vijiji vyao”, ameeleza na kuongeza kuwa,
“Miradi ya ajira za muda zitawafundisha Wahadzabe kujituma kufanya kazi ambazo zinachangia maendeleo ya jamii huku kazi hizi zikiwa kama darasa la wao kujifunza kwa vitendo kuwa kama anaweza kwa mfano kushiriki kujenga bwawa basi anaweza kufanya jambo kubwa katika familia au maisha yake”, amesisitiza Dkt Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na Wahadzabe waliokuwa wakijiandaa kupokea fedha kutoka Mpango wa Tasaf katika kijiji cha Munguli Wilayani Mkalama, Dkt Nchimbi amewatahadharisha kutofanya matumizi mabaya ya fedha hizo.
Walengwa wa Tasaf wa kijiji cha Singa Wilayani Mkalama wakimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (hayupo pichani) alipowatembelea kushuhudia ujenzi wa bwawa walilolijenga katika mpango wa ajira za muda za Tasaf.
Bwawa lililopo katika kijiji cha Singa Wilayani Mkalama lililojengwa na walengwa 246 wa Tasaf katika mpango wa ajira za muda, bwawa hilo linaujazo wa mita 5777.6 ambalo litasaidia upatikanaji wa maji na uanzishwaji wa kilimo cha umwagiliaji, Dkt Nchimbi ameagiza halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kuweka miundombinu ya kunyweshea maji mifugo kutoka katika bwawa hilo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...