WATUMIAJI wa vyakula na dawa wanatakiwa kuangalia zaidi ya usalama wa vyakula  ,Dawa  pamoja na vipodozi katika kulinda afya zao.

Hayo aliyasema Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza wakati wa maonesho ya bidhaa za viwanda vya ndani yaliyoahirishwa jana, amesema kuwa TFDA  kazi ya kubwa ni kudhibiti kuhakikisha walaji wanalindwa.

Akifafanua kuhusu vipodozi amesema licha ya kupiga marufuku vipodozi ambavyo vimetengenezwa na kemikali ambazo zinamadhara bado kuna baadhi ya Watanzania wamekuwa wakivitumia na matokeo yake kupata athari mwilini.

Amesema  athari zitokanazo na vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku ni nyingi ikiwamo ya kansa ya ngozi huku akisisitiza atakakutwa akiuza vipodozi vilivyopigwa marufuku hatua za kisheria zitachukulia dhidi yake.

Amesema TFDA itaendelea kutoa elimu kwa Watanzania itakayosaidia kuwaondoa kupata athari za kiafya kwa kutumia vyakula, dawa na vipodozi ambavyo havina ubora.
 Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudensia Simwanza akizungumza na wateja waliotembele maonesho ya bidhaa za viwanda vya ndani yaliyofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya vipodozi bandia ‘Fake’vilivyo katika maonesho ya viwanda ndani katika maonesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika maonesho ya bidhaa za viwanda yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakisubiri picha kwa ajili ya vitambulisho  vya taifa katika maonesho ya bidhaa za viwanda yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...