Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limepitisha majina manne ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kuwa makamishna wa michezo mbalimbali inayoandaliwa na CAF.

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zilizotoa Makamishna wanne ambayo ni idadi ya juu hakuna nchi iliyozidisha idadi hiyo ambayo ni kwa kipindi cha kutokea mwaka 2018 mpaka 2020.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF waliopata nafasi hiyo ni Makamu wa Rais Michael Wambura,Ahmed Mgoyi,Amina Karuma na Sarah Tchao.

Wambura kwa upande wake amechaguliwa kutokana na kufanya vizuri katika aiku za nyuma wakati Mgoyi amepata nafasi hiyo kwa kufanya vizuri kama mechi kamishna wa michezo ya CECAFA nao Karuma na Tchao wameipata nafasi hiyo kutokana na mkakati wa CAF kuanza kuwajengea uwezo viongozi wanawake vijana.

Kuteuliwa kwa viongozi hao wa TFF ni muendelezo CAF kuteua viongozi wa TFF kwenye kamati mbalimbali itakumbukwa hivi karibuni Rais wa TFF aliteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya fainali za Africa kwa wachezaji wa ndani CHAN inayoendelea nchini Morocco lakini pia akiteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya ufunguzi iliyowakutanisha wenyeji Morocco na Mauritania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...