NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ametuma salamu za rambi rambi kwa familia ya mtumishi wa Chama hicho Zanzibar Marehemu Bi. Nakia Khamis Abdalla aliyefariki leo Januari 25,2018.

Bi. Nakia amefariki dunia akiwa nyumbani kwake mtaa wa Sogea Zanzibar baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Katika Salamu zake Dk. Mabodi amesema CCM Zanzibar imepokea taarifa ya kifo cha mtumishi huyo kwa Mshutuko, Majonzi na Simanzi kubwa, kwani Marehemu enzi za uhai wake alikuwa Mwadilifu aliyefanya kazi kwa bidii na ubunifu wa hali ya juu katika utumishi wake.

Pamoja na hayo alitoa pole kwa familia Wanachama, Viongozi na Watendaji Wote wa CCM, Marafiki pamoja na Jamaa wa karibu walioguswa na msiba huo, na kuwaomba waendelee kuwa na uvumilivu katika kipindi chote cha msiba huo.

“ Marehemu alikuwa ni mfano wa kuigwa enzi za uhai wake hasa kwa kujitolea na kukipigania Chama cha Mapinduzi muda wote wa uhai wake, hivyo tumepoteza mtu muhimu sana ndani ya Chama na Taifa kwa ujumla.

Pia nawaomba watumishi na wanachama na Familia ya Marehemu kuwa na Subra katika kipindi hiki kigumu cha Msiba huo, na tuendelee kumuombea dua mwenzetu ili Mwenyezi Mungu amuweke pahala pema peponi Amin.”, alieleza Dk. Mabodi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...