Rais wa Marekani Donald Trump amemuomba Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) kufikisha salamu zake kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU.

Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi pambizoni mwa mkutano wa viongozi na watu mashuhuri kuhusu uchumi na biashara duniani.
Mkutano huo wa Kagame na Trump umetokea wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kuyaeleza mataifa ya Afrika kama "machafu" au mataifa ya "mabwege".
Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana.Bw Trump amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyaelezea mataifa ya Afrika.

Hata hivyo alikiri kwamba alitumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.
Lakini katika mkutano wake na Kagame pambizoni mwa Mkutano wa Uchumi wa Dunia mjini Davos, Trump hajaonyesha dalili zozote za majuto kuhusu tamko lake la awali kuhusu Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...