Na John Stephen wa Muhimbili
Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili leo limefanya kikao chake cha 18 na kujadili agenda mbalimbali katika kikao hicho ikiwamo maslahi kwa wafanyakazi.
Katika kikao hicho ambacho kimefanyika  Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti wake Profesa Lawrence Museru, baraza limepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17.
Kabla ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo, Katibu wa TUGHE mkoa  Bw. Gaudensi Kadyango amezungumzia umuhimu wa majadiliano mahala pa kazi kuhusu mwajiri na chama cha wafanyakazi ili kuondoa malalamiko na kufanya kazi kwa tija.
Amesema majadiliano ni sehemu ya kazi  hivyo pande zote mbili zinatakiwa kuwa na busara kwa kila mmoja kusikiliza hoja ya mwenzie.
Mada nyingine iliyowasilishwa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira , Vijana na wenye ulemavu ni umuhimu wa utamaduni katika kuinua viwango vya utendaji wa kazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akielezea mada hiyo Bi.Tulia Msemwa amesema utamaduni wa taasisi unatakiwa uangaliwe kwa makini hasa katika Dunia hii ya utandawazi ili kuruhusu tamaduni nyingine mpya kama zile zinazohusika na ufumbuzi, udadisi na ubora wa kazi na kuwajali wateja.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akifafanua jambo kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Muhimbili. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo, Eneza Msuya na kulia ni wawakilishi kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Zaria Mmanga na Pascal Magesa.

 Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakifuatilia mkutano huo ambao umejadili mada mbalimbali yakiwamo maslahi ya wafanyakazi na utekelezaji wa shughuli za hospitali.
 Mkurugenzi  wa Rasilimali Watu katika hospitali hiyo, Makwaia Makani akieleza jambo kwenye mkutano huo. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo, Eneza Msuya na wengine ni wajumbe mkutano huo.
 Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, Dkt. Frank Masao akiuliza swali.

Wajumbe wakifuatilia mkutano huo Leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...