*Wanafunzi wa kike kuanzia darasa la nne kupewa chanjo
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
TAASISI
ya Saratani ya Ocean Road imesema imekuwa ikipokea wagonjwa wapya wa
saratani 50,000 kila mwaka huku ikielezwa saratani ya shingo ya kizazi
ndio inayoonekana kuongeza.
Pamoja na hali
hiyo, imeelezwa jitihada mbalimbali zinafanywa na Serikali kwa
kushirikiana na taasisi hiyo ambapo wameweka mkakati wa kuhakikisha
wanafunzi wa kike waliopo kuanzia dasara la nne nchi kote watapatiwa
chanjo itayakayosaidia kuwakinga na aina hiyo ya saratani.
Hayo
yamesemwa leo (jana) jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Kinga
katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.Chrispin Kahesa wakati wa
semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa wahariri wa vyombo vya habari
nchini.
Lengo la semina hiyo ilikuwa ni kutoa
elimu kuhusu ugonjwa wa satarani, hali ilivyo kwa sasa nchini, sababu
zinazosababisha ugonjwa huo na pamoja na jitihada zinazochukuliwa
kupunguza kasi ya saratani nchini.
WATANZANIA 50,000 KILA MWAKA HUPATA SARATANI
Akizungumzia
ugonjwa huo ,Dk.Kahesa amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya
Duniani(HWO), Tanzania kila mwaka kunakuwa na wagonjwa wapya 50,000 wa
saratani na hivyo unaweza kuona ukubwa wa ugonjwa huo nchini kwetu.
"Kila
mwaka Tanzani wagonjwa wapya wa saratani ni 50,000.Ni idadi kubwa
ambayo lazima tuweke mikakati ya pamoja kuhakiksha tunapunguza idadi
hiyo na ukweli tunaweza."Ni suala la kuamua tu
kuanzia mtu mmoja mmoja, familia na Watanzania kwa ujumla kwani baadhi
ya sababu zinazosababisha ugonjwa huu tunaweza kuzikwepa.
"Baadhi
ya sababu zinazosababisha saratani ni uvutaji sigara, pombe, vyakula
vyenye mafuta mengi, kutofanya mazoezi ya mwili,unene na taka
sumu.Hivyo ukiangalia hizo sababu unaweza kuziepuka na ukishindwa zote
basi chagua hata sababu mbili zieupuke,"amesema.
Amefafanua
zipo saratani ambayo hutokana na kirusi ambacho hubebwa na mwanaume na
kisha kukiacha kwa mwanamke kupita tendo la ndoa na aina hiyo ya kirusi
ndicho kinachosababisha saratani ya shingo ya kizazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...