Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto kwa kushirikiana na team yake ya Mpoto Foundation alitembelea kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa na madrasa ya Tidaiya iliyopo Tandale.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akikabidhi zawadi hizo, Mpoto alisema lengo kubwa la kutoa zawadi hizo ni kusaidia malezi ya watoto katika vituo hivyo ili wakue wakiwa katika maadili mazuri.
“Nimeamua kugawana na watoto kidogo nilichojaliwa nacho ili waweze kufurahi lakini pia kuwasaidia katika makuzi hasa kwenye suala zima la kidini na maadili.” alisema Mpoto.
Aidha Mpoto aliongeza kuwa kutokana na mambo mengi yanayoendelea kwa sasa nchini na duniani kote, kuna uwezekano kwa watoto kukua bila misingi mizuri ya dini, heshima na uzalendo kama wasipoandaliwa mazingira mazuri.
Ili kuhakikisha hilo halitokei, Mpoto amesema imekuwa sababu kubwa iliyompelekea kujitolea zawadi hizo ambapo kwa yeye ni kuufungua mwaka 2018 akiwa na thawabu kutoka kwa watoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...