NIDHAMU mpya katika ukusanyaji na matumizi ya fedha za umma na dhamira ya dhati ya kutekeleza ahadi kubwa kwa faida ya wananchi vimesaidia Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kutekeleza kwa mafanikio miradi mbalimbali mikubwa ya kitaifa. Baadhi ya mambo yaliyotekelezwa na kufafanuliwa leo kwa wanahabari ni kama ifuatavyo: 

Hali ya Uchumi

Kama alivyoeleza Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango siku chache zilizopita, tunawahakikishia watanzania kuwa hali ya uchumi wa nchi yetu inaendelea kuwa imara kwa kiasi cha kuziridhisha taasisi mbalimbali za kimataifa.

Ripoti za Shirika la Fedha Duniani (IMF), Benki ya Dunia (WB) na Taasisi ya Goldman Sachs ya Marekani zimetabiri kuwa wakati uchumi wa dunia utakua kwa wastani wa asilimia 3.0 hadi 4.0, ukuaji wa uchumi wa Tanzania unatajwa kuendelea kuwa kati ya nchi tano bora za Afrika ukitarajiwa kukua kwa asilimia 6.5 hadi 7.0 katika mwaka 2018.

Ahadi ya Kuhamia Dodoma

Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuonesha nidhamu ya kuahidi na kutekeleza ahadi ya kuhamia makao makuu, Dodoma. Kufikia mwishoni mwa Desemba, 2017, viongozi waandamizi wa Serikali wameshahamia Dodoma. Rais mwenyewe akitarajiwa mwaka huu.

Mbali na viongozi, jumla ya wafanyakazi 3,671 kutoka wizara na taasisi mbalimbali za umma wameshahamia makao makuu Dodoma. Awamu inayofuata baadaye mwaka huu itahusisha wafanyakazi wengine 2,460. Sekta binafsi ichangamkie fursa za Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati alipotoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kutolea ufafanuzi wa masuala kadhaa, Pichani kushoto  Mkurugenzi Msaidizi upande wa usajiri wa Magazeti Ndugu Patric Kipangula  na Kulia Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus 
Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari mapema leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli. Pichani kushoto ni  Mkurugenzi Msaidizi upande wa usajiri wa Magazeti Ndugu Patric Kipangula  na Kulia Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus .PICHA NA MICHUZI JR.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...