NA WAMJW-MTWARA

SERIKALI Kupitia Wizara ya Afya imeagiza Kampuni ya Ujenzi na Uhandisi Nadhra kumalizia kazi ya kurekebisha kasoro zilizotokana na ujenzi katika majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara ( NTC) na Chuo cha Maafisa Tabibu mkoani humo (COTC) ili kuweza kudahili wanafunzi wengi zaidi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Castro Simba wakati wa ukaguzi wa majengo hayo mkoani Mtwara.

“Majengo haya yalimalizika Desemba 2016 tukatoa kipindi cha mwaka mmoja kujiridhisha na ubora wake lakini kuna baadhi ya maeneo hayajakidhi ubora hivyo mkandarasi anatakiwa kurekebisha ndani ya mwezi mmoja” alisema Bw. Simba.

Aidha Bw. Simba amesema kuwa mradi huo wa kupanua, kukarabati na kujenga majengo hayo yanafanyika katika vyuo vitano nchini ikiwemo Hospitali ya Kairuki Dar es salaam, Bagamoyo, Chuo cha Uuguzi Mtwara (NTC), Chuo Cha Maafisa Tabibu (CoTC) na Chuo cha St. Bakhita cha Sumbawanga.
Mshauri elekezi wa mradi wa upanuzi na ujenzi katika Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc Arch. Benjamini Kasiga aliyevaa fulana ya bluu akiwakilisha mada katika kikao kifupi kilichofanyika chuoni hapo wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanywa na jopo la Wakaguzi kutoka Wizara ya Afya Mkoani Mtwara.
Mkandarasi kutoka kampuni ya Ujenzi na Uhandisiz Nandhra wa kwanza kushoto akiwapa maelezo baadi ya wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya Afya wakati wa ukaguzi wa majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc uliofanyika leo mkoani humo. 
Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha kusanifu Majengo Wizara ya Afya Arch. Daniel Mwakasungura aliyevaa shati jekundu akiangalia moja ya sehemu ya jengo la Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanyika leo mkoani humo, katikati ni Mratibu wa ujenzi huo Dkt. Joachim Catherine na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizara ya Afya Bw. Castro Simba.
Jengo la wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo lipo kwenye ujenzi bado ambapo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la ujenzi wa Hospitali hiyoni kuweza kutoa huduma za kibingwa.Picha Na Wizara ya Afya-MTWARA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...