TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania( Takukuru) wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kwa upande wao wamekwisha kamilisha upelelezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa rais Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) Jamali Malinzi na wenzake.
Mbali na Malinzi wengine ni, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine(46) na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo Mwanga(27).
Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leonard Swai amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba,leo mahakamani hapo kuwa upelelezi katika shauri hilo kwa Takukuru umeishakamilika na hadi Jumatatu jalada la kesi hiyo litakuwa limekwisha rejeshwa (DPP).
Awali, Swai alidai mahakamani hapo jalada la kesi hiyo lilipelekwa kwa DPP ambapo alilipitia na kurirejesha Takukuru kwa maelekezo ambapo wamekwisha yafanyia kazi.Kutokana na taarifa hiyo, Hakimu Simba ameahrisha kesi hiyo hadi Februari 8, mwaka huu.
Washtakiwa hao, walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29, mwaka 2017, wakikabiliwa na mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...