Na: Veronica Kazimoto.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepongezwa kwa kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa ofisi za Serikali na Asasi za Kiraia kwa ajili ya kuongeza ufahamu na kuwa mabalozi wa masuala yanayohusu kodi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu ya kodi kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) yaliyofanyika leo ofisini hapo,  Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Bw. Edwin Rutageruka amesema TRA inastahili kupongezwa kwa kazi inayoifanya ambayo imepelekea kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.
"Ni dhahiri kwamba, sasa hivi  TRA inafanya kazi kubwa ya ukusanyaji wa mapato na kutoa elimu ya kodi kwa vikundi na taasisi mbalimbali, hivyo, fursa hii tuliyoipata tuitumie vizuri ili kuongeza uelewa wa kutosha kuhusu kodi ili tuwe  mabalozi wazuri kwa wengine", amesema Rutageruka.
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania  Bi. Rose Mahendeka, akiwasilisha mada ya Kodi na Mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya mwaka 2017 amesema,  kila mwananchi anajukumu la kudai risiti kila anaponunua bidhaa na kila mfanyabiashara anatakiwa kutoa risti kila anapofanya mauzo.
 Afisa Muelimishaji Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Rose Mahendeka akiwaelimisha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Kodi na Mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2017/18 katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018.
 Msaidizi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Chama Siriwa akiwasilisha mada mbele ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Kodi ya Majengo, katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018.
Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Valentine Baltazar akiwasilisha mada mbele ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Taratibu za Kiforodha, katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...