WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inakamilisha ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara iliyoanza kujengwa mwaka 1980.
Atoa kauli hiyo leo (Jumatatu, Januari 15, 2018) wakati alipokagua ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kuwasili mkoani Mara kwa ajili ya ziara yake ya kikazi.
Waziri Mkuu amesema Serikali itakamilisha ujenzi wa jengo hilo kwa awamu, ambapo wataanza na eneo la mapokezi na vyumba vya madaktari.
Amesema Serikali imedhamiria kuboresha huduma za afya nchini, hivyo amewaomba wananchi waendelee kuiamini na kushirikiana nayo.
Waziri Mkuu amesema tayari Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 ili ujenzi uendelee. Ujenzi huo ulianza mwaka 1980, ulisimama mwaka 1987 kuanza tena 2010.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudencia Kabaka baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma kuanza ziara mkoani humo Januari 15, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua majengo ya Shule ya Secondari ya Ufundi Musoma akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara Januari 15, 2017.Serikali imetoa shillingi bilioni 1.28 kwa ajilli ya ukarabati huo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Samweli Kiboyi. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Mutta Venance.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya bweni la Shaban Robert wakati alipokagua ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara Januari 15, 2017. Serikali imetoa zaidi ya shilling bilion 1.28 ili kugharimia ukarabati hou.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kwangwa mjini Musoma akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 15, 2017. Kulia wake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...