NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameteketeza Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242 baada ya wavuvi kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayni Sengerema mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa uteketezaji wa nyavu hizo, Ulega aliwapongeza wavuvi hao kwa hatua hiyo walioichukua huku akikazia msimamo wa serikali wa kupambana na uvuvi halamu. Pamoja na kuwapongeza huko,Ulega aliwasisitiza wavuvi hao kuzingatia sheria na taratibu za uvuvi ili kuzilinda rasilimali hiyo, ambayo ilikuwa inaelekea kutoweka.

"Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa samaki, wazazi walikuwa wamebaki asilimia nne, wenye hadhi ya kuvuliwa kwa maana ya sentimita 50 hadi 85 wamebaki asilimia tatu na wachanga wamebaki asilimia 93, na kama uvuvi huu ungeendelea maana yake ziwa lingebaki jangwa," alisema Ulega

Waziri Ulega aliwataka wavuvi hao kununua nyavu zinazokubalika kwenye viwanda ambavyo vinauza nyavu hizo,  badala ya kuendelea kutumia nyavu zisizoruhusiwa kwani watapata hasara kwa kuteketezewa na wengine kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.

kwa upande wake kiongozi kazi maalumu mkoa wa kioparesheni Sengerema, Charles Lwekaza alisema baada ya kufanya operesheni hiyo iliyoanza mapema Januari mwaka huu, baadhi ya wavuvi waliamua kuzisalimisha nyavu hizo wenyewe bila shuruti.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega  akiongoza shughuli za kuteketeza Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242  baada ya wavuvi kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza
 .Wavuvi wakisogeza  Nyavu haramu 242 zenye thamani ya Sh Mil.242  eneo la kuchomea  baada ya kuzisalimisha wenyewe katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi  katika kisiwa cha Zilagula  kilichopo halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.Picha na Emanuel Massaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...