Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo, William Lukuvi ameanza ziara mkoani Mwanza kwa lengo la kusikiliza wananchi wenye kero na changamoto mbalimbali katika eneo la ardhi. 

Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo inaeleza kuwa Waziri Lukuvi atafanya ziara wilayani Ilemela na Nyamagana na akiwa huko atakagua eneo la Polisi Kigoto lililovamiwa na wanachi. 

Pia atakagua maeneo ya Ilemela Mahakamani, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), na Uwanja wa Ndege. 

"Waziri Lukuvi atakuwa kwenye kuanzia leo Januari 25 hadi 27 mwaka guy ambapo atakagua maeneo kadhaa yenye migogoro ya ardhi, "imesema taarifa hiyo. 

Waziri Lukuvi pia atasikiliza kero za wananchi kuhusu mchakato wa urasimishaji wa makazi, Buguku katika kata ya Buhongwa.

Pia kuhamasisha kwa kutoa hati na kusikiliza kero za wananchi kuhusu urasimishaji eneo la Nyasaka wilayani Ilemela. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...