MBUNGE wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu amekabidhi chakula na vifaa vyengine kwa ajili ya kuisaidia timu ya African Sports ya Jijini Tanga kujikimu katika kambi yao iliyopo maeneo ya Donge Tanga.

Msaada huo umefika wakati muafaka ambapo timu hiyo inajiandaa kuelekea michezo yao miwili iliyobakia ya ligi ya Taifa Daraja la Pili inayomalizika ndani ya wiki mbili.Miongoni mwa vitu alivyokabidhi ni pamoja na Mchele kg 100,Unga wa ngano kg 50,Unga wa sembe kg 100,Maharage kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia lita 20,chumvi,sabuni na dawa za meno ambavyo vilikabidhiwa na Khatibu Kilenga kwa niaba ya Waziri Ummy.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi kwa niaba ya Waziri Ummy ,Kilenga aliwaambia wametakiwa heri katika michezo miwili iliyosalia kwenye michuano hiyo.Aidha pia ni matumaini yake kwamba katika michezo hiyo timu hiyo itaweka bidii kubwa kuhakikisha inashinda .Naye kwa upande wake,Katibu wa timu ya African Sports,Ismail Masoud alimshukuru Waziri Ummy kwa sapoti kubwa anayoionyesha na kwamba sasa wachezaji wamepata hari na nguvu ya kushinda mechi mbili zilizobakia.

Alisema mipango ya kushinda michezo hiyo iliyobakia ni mizuri ili kuhakikisha hawashuki daraja huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia timu hiyo kwani ni ya wananchi."Tanga ina enye ,na enye ni sisi,Shime wana Tanga'Tanga Kwanza.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Mwakilishi wa MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu,Khatibu Kilenga kushoto akimkabidhi unga nahodha wa timu ya African Sports ambapo kiongozi huyo alitoa mchele kg100,unga wa sembe kg 100,Ngano kg 50,maharage kg 50,sukari kg 50,mafuta ya kupikia lita 20,chumvi ,sabuni na dawa za meno

Sehemu ya vitu vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu

Katibu wa Klabu ya African Sports,Ismail Masoud katika aliyeshika funguo akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo ambao utakuwa chachu ya timu hiyo kumaliza ligi wanayoshiriki kwa ushindi 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...