Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Waziri wa Afya Wanawake,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  ameshtushwa na wingi wa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke na kuagiza katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya utaratibu wa kuongeza madaktari ili kutoa huduma kwa ufanisi.

Waziri Ummy ametoa maagizo hayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea Hospitali zote za Mikoa za Rufaa ambazo Rais Magufuli ameagiza zianze kuhudumiwa na Wizara ya afaya badala ya halmashauri husika.

"Nimetembelea hapa nimejionea mwenyewe kuwa  na msongamano mkubwa sana hapa kiasi cha Daktari mmoja kuweza kuhudumia wagonjwa 300 kwa siku kwa mujibu wa maelezo ya Mganga mkuu wa hospitali hii jambo ambalo  linahitaji kushughulikiwa mapema hivyo namuagiza katibu mkuu kuweza kuongeza madaktari hapa hili waweze kuwahudumia Wananchi kwa wakati"amesema Ummy.

Waziri Ummy pia alimwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke kuhakikisha kuwa anaweka X Ray katika hospitali zilizopo chini yake hili kuweza kupunguza wimbi lka wagonjwa wengi amabo ukimbilia katika Hospitali hiyo.
 Waziri wa  Afya Wanawake Jinsia Wazee na  Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na Mmoja wa Wanawake  waliojifungua katika Hospitali ya  Rufaa ya Temeke na kubaini kuwepo kwa idadi kubw aya wagonjwa kuliko kawaida kutokana na Daktari mmoja kihudumia wagonjwa zaidi ya 300 katika OPD.
 Waziri wa Afya Wanawake Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizunguma na watu waliojaa katika Mapokezi ya Hospitali ya  Rufaa Temeke amabo wanahudumiwa na madkatari wachache.
 Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Dk Amani Malima akitoa maelezo kwa  Waziri wa Afya Wanawake Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  kwanini hospitali hiyo ina wagonjwa wengi .
 Sehemu ya Umati wa Wagonjwa waliofurika katika Hospitali ya Rufaa Temeke.
 Waziri wa Afya Wanawake Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Temeke Dr. Amani Malima akizungumza na Waandishi wa Habari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...