Na Agness Francis, Globu ya Jamii

MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC  kesho kukutanaa uso kwa uso na AzamFc  katika  kukamilisha mzunguko  wa kwanza,mchezo utakaochezwa Uwanja  wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza Msemaji Mkuu  wa Yanga SC  Dismas Ten leo Katika Makao makuu yao amesema wachezaji wapo fiti kuelekea mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki  kuwa wamejipanga kuondoka na ushindi  dhidi ya Azam FC  kuachilia mbali kuwa watakuwa wageni wa mchezo huo mashambulizi yatakuwa ya kutosha katika kuonesha uwezo mkubwa walionao. 

Aidha amesema kikosi hicho kitawakosa wachezaji wake nyota  katika mtanange huo ambao ni Thabani Kamusoko, Amiss Tambwe, Yoana Mkomola, Pato Ngonyani, Donald Ngoma, Abdalah Shaib  ambao wako majeruhi pamoja na Pius  Biswita ambaye anatumukia adhabu ya kadi 3 za njano.  

Pia Msemaji Huyo amesema kuwa "katika mchezo wao wa kesho watamkosa Kocha Msaidizi  shedrack  Nsajigwa ambaye amepa msiba,"amesema Dismas. 

Pia Dismas amesema kwa siku ya kesho Kocha Mkuu George Lwandamina atarejea katika benchi la ufundi kuongoza kikosi chake kama ilivyokuwa hapo awali ikiwa kibali chake kipo hatua za mwisho kukamilika

Mzambia huyo alikuwa akikaa jukwaani wakati wa mechi za Mabingwa hao zikichezwa kwa sababu ya  kumalizika kwa  muda wa kibali chake cha kufanya kazi hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...