BENKI ya TPB imeungana na taasisi ya Savings at the Frontier (SatF), kwenye mradi utakaogharimu kiasi cha dola Milioni Moja.
Mradi
huo unaoitwa “Digitalizing Informal Savings Mechanisms” utaendeshwa kwa
kipindi cha miaka mitatu (3) ambapo TPB inatarajia kuwaunganisha kwenye
mfumo rasmi wa kifedha wateja wapya laki Mbili na nusu hadi kufikia
mwaka 2020, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Bw. Sabasaba Moshingi
amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 16,
2018.
Kitangaza mradi huo mbele ya waandisahi wa habari, Bw. Moshingi alisema, mradi huo utaanzia Mkoa wa Ruvuma, na baadae kupelekwa Mikoa ya Mtwara, Lindi, Njombe, Iringa na Morogoro.
“Watanzania wengi waishio kwenye mikoa ya pembezoni, hususani wenye vipato vidogo wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa huduma za kifedha. Kupitia ushirikiano huu na SatF, TPB itawawezesha wananchi kupitia makundi au mtu mmoja mmoja, kujiwekea akiba kupitia teknolojia rahisi na salama isiyowalazimu kwenda kwenye tawi la benki ili kupata huduma hizo za kifedha. Njia hii itawawezesha wananchi kutatua changamoto zao mbalimbali za kifedha na pia kuwaingiza kwenye mfumo rasmi wa kiuchumi.

Meneja wa mradi kutoka programu ya SatF, Bw. Steve Peachey(kushoto), akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Bw. Sabasaba Moshingi.

Bw. Moshingi akifafanua jambo huku Bw. Peachey, (wakwanza kushoto), na Bw.Ignas Jacob kutpoka SatF, wakisikiliza.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Bw. Sabasaba Moshingi, (kulia), akipeana mikono na Meneja Mradi kutoka programu ya SatF, Bw. Steve Peachey, wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari makao makuu ya TPB jijini Dar es Salaam Februari 16, 2018.BENKI ya TPB imeungana na taasisi ya Savings at the Frontier (SatF), kwenye mradi utakaogharimu kiasi cha dola Milioni Moja. Mradi huo unaoitwa “Digitalizing Informal Savings Mechanisms”
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...