Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
VIGOGO 27 kutoka chama cha wananchi (CUF) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)waliotikisa uchaguzi mkuu 2015,maeneo mbalimbali wilayani Rufiji Mkoani Pwani ,wamevihama vyama vyao na kukimbilia CCM.
Aidha wanachama wapya 120 wamejiunga na CCM wilayani Rufiji huku wengine 211 wamejiunga na chama hicho wilayani Mkuranga.Hayo yalijiri katika msafara wa Chama Cha Mapinduzi mkoani Pwani ,kuadhimisha miaka 41 ya CCM katika wilaya hizo ambapo pia walishiriki katika shughuli za kimaendeleo.
Akiongea kwenye maadhimisho hayo ,Utete ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rufiji ,Kaswakala Mbonde alisema wapambe na baadhi ya viongozi hao wa upinzani wamekikubali chama tawala kutokana na mabadiliko ya maendeleo na uchumi yanayofanywa na serikali yake .
Alisema serikali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi makubwa katika sekta ya miundombinu ,afya,elimu,uwekezaji hivyo wapinzani hawana la kukosoa.Pamoja na hayo ,Mbonde alieleza wapo wanachama wengine wapya 255 waliojiunga na jumuiya ya wanawake (UWT) na 25 wamejiunga jumuiya ya wazazi Rufiji .
Mwenyekiti Wa kitongoji cha Nyangwai kata ya Chemchem aliyekuwa (CUF) Jafar Mpunjo alisema ,wapinzani kazi yao kukosoa na kubeza lakini kwasasa wanakosa la kukosoa .Mwingine aliyehamia CCM Ashura Sultan alisema ,upinzani ukifika 2019-2020 utakuwa umekufa .

ALIYEKUWA mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Nyangwai Kata ya Chechem wilayani Rufiji ,mkoani Pwani mwenye miwani nyeusi ,ameiacha nafasi hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 41 ya CCM huko Utete ,ambapo msafara wa CCM Pwani ,ulipokea wapinzani 27 na wanachama wapya 120 katika maadhimisho hayo.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Utete wilayani Rufiji wakisheherekea baada ya kupokelewa wapinzani 27 waliotikisa uchaguzi mkuu 2015 wilayani hapo,katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 41 ya CCM ,ambapo msafara wa CCM Pwani ,ulipokea pia wanachama wapya 120 katika maadhimisho hayo.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani Ramadhani Maneno akikabidhi kadi kwa wanachama wapya katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 41 ya CCM huko Utete ,pia alipokea wapinzani 27 na wanachama wapya 120 katika maadhimisho hayo
Wakila kiapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...