Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi
Waziri wa Nishati, Mh. Dk. Medard Kalemani Februari 15 mwaka amefanya ziara wilayani Kishapu ambapo amezindua ujenzi wa miradi ya kusambaza umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Akiwa kwenye vijiji vya Negezi na Mwamashele, Dk. Kalemani alimuagiza mkandarasi anajenga mradi huo kukamilisha kwa wakati na kuviunganisha vitongoji vyote kwa umeme bila kuruka nyumba.
Alimuagiza kufikia Aprili mwaka huu kazi ya kusambaza nishati hiyo iwe imekamilika ili wananchi wanufaike na huduma hiyo na hivyo kuweza kuutumia kwa shughuli za maendeleo.
“Mkandarasi ongeza kasi hakuna kulala kumaliza mradi huu hatutaki wananchi wakwame na tunahakikisha vijiji vyote 118 vinapata huduma ya umeme, nakuagiza ndani ya siku 40 hapa Mwamashele umeme uwe umewaka,” alisema.
Dk. Kalemani aliwataka wananchi hao kuutumia umeme huo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi zikiwemo kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili kujipatia kipato.
Pia aliwahimiza kuwa tayari kupokea nishati hiyo katika nyumba zao kwa kutandaza nyaya na kuwataka kuitunza miundombinu inayosambaza umeme ikiwemo, nguzo, nyaya na transifoma ili isaidie kutokatika kwa huduma hiyo.
Waziri
wa Nishati, Mh. Dk. Medard Kalemani akizungumza na wananchi katika
kijiji cha Negezi ambako aliwasha umeme katika taasisi ya Serikali
ambako tayari mradi huo ulijengwa awamu iliyopita.
Mbunge
wa Kishapu, Seleman Nchambi akizungumza katika mkutano wa hadhara
wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati kijiji cha Negezi.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio kwenye shughuli hiyo.
Sehemu
ya nguzo zikiwa tayari zimewasili kijiji cha Negezi kwa ajili ya kuanza
kusimikwa wakati wa ujenzi wa mradi huo vijiji mbalimbali.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...